AMKA JITAMBUE

 

Robison Robison Author
Title: NAMNA YA KUKABILI HALI MBAYA KAIKA MAISHA ...2
Author: Robison
Rating 5 of 5 Des:
katika makala iliyo pita tuliweza kuona ni jinsi gani unaweza ukaifundisha akili yako kupokea taarifa kupitia FIKRA CHANYA, fikra chanya ni ...
katika makala iliyo pita tuliweza kuona ni jinsi gani unaweza ukaifundisha akili yako kupokea taarifa kupitia FIKRA CHANYA, fikra chanya ni uwezo wa kutafsiri mambo na kupata uzuri ama sababu ya kutokea jambo husika. tafsri juu ya matukio ndiyo imekutengeneza katika hali ya maisha tunayo kuona nayo leo, ukitaka kubadilika au kuanza kupokea matokeo tofauti badilisha namna ambavyo unatafsiri mambo yanayo kutokea katika amisha yako.

kwanza itakuwa ni vema tukajiuliza akili inatoa wapi tafsri, kwasababu kila kitu kina chanzo. akili zetu zinajifunza namna ya kuchukuliana na mambo kulingana na namna ambavyo tumejifunza kutoka maeneo mbali mbali, inaweza ikawa watu walio tuzunguka, kutokana na matukio tunayo yaona, na kulingana na uzoefu wa watu wengine mambo yote haya yana athiri kwa kiwango kikubwa namna ya kuchukuliana na mambo.

na hakuna kitu kigumu katika maisha kama kukabiliana na matokeo ambayo hatukuyatarajia katika maisha  yetu, kwa mfano kama ulitarajia kupata faida kwenye biashara flani lakini ikatokea ukapata hasara huwa inashtua na kukatisha tamaa, na hapo ndipo tunapo kuta watu wenye ujasiliri wa kuendelea na wale wanao kata tamaa kuelekea kufikia mafanikio yao.

chanzo kikubwa kinachopelekea kushindwa kufanikiwa au kukabiliana na changamoto hizo kutokana na ukweli kwamba akili zetu zinatawaliwa zaidi na FIKRA HASI fikra ambazo zinatuonyesha ubaya wa jambo ila siyo uzuri wake, fikra ambazo zinatufanya tuwe wepesi kulalamika na kushindwa kukabiliana na hali zilizopo mbele yetu matokeo yake tunabaki tukiumia ikiwa uwezo wa kutatua tunao.

zifuatazo ni baadhi ya njia za kukabiliana na hali hizo kwa mtazamo wa kisaokolojia kwa kubadilisha mtizamo wako wa ndani kwasababu huko ndiko kwenye injini ya maisha yetu,.

kubali kwamba wewe ndiyo chanzo cha matatizo yote, ukitaka uone matokeo mazuri na uwe na uwezo wa kukabiliana na matukio yanayokutokea katika maisha ni lazima ukubaliane na ukweli huo ili uache kulalamika. kama umeishi kwenye maisha ya kulalamika muda mrefu na hufurahii aina hiyo ya maisha anza sasa ku ACCEPT REALITY, kubaliana na ukweli kwamba wewe ndiyo chanzo cha aina ya maisha unayo ishi sasa na wewe ndiyo wmenye tiba ya kuyaondoa matatizo hayo hakuna mwingine.

kuna hii kauli wanasema "wabongo wanaongea sana" usiwe mtu wa aina hiyo kwasababu mtu anaeongea sana ni yule anae lalamika na kama unalalamika ujue unamambo mengi yanayokukabili ambayo umeshindwa kuya tatua. ukiwa na matatizo mengi yaliyo kuzunguka na huna uwezo wa kuyakabili basi ni lazima uishi kuwa muongeaji mzuri na mlalamishi.

kuanzia sasa kubali kwamba wewe ndiyo chanzo cha matokeo au matukio unayo yaona sasa, usijidanganye mtu hawezi kukudharau kama wewe hujaruhusu hilo, unaweza ukaruhusu kwa namna mbali mbali ikiwemo kwa muonekano mavazi yako, mazungumzo yako. nk hivyo basi mambo yote yanatokana na namna ambayo tumejipanga kukabiliana na matukio mabaya katika maisha yetu.

itaendelea............
tutakuwa na online seminar,
itakayo anza 1/4/2016
jisajili sasa kupitia +255 653 206 053
ada 1000/
karibu..

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top