Leo tutajadili njia utakazo weza kuzitumia au maandalizi unayo akiwa kuyafanya katika kila siu za maisha yako ili uweze kukabiliana na matukio yasiyo tarajiwa,
kumbuka kuweka akiba, akiba ni kitu muhimu sana katika kuweka uzio au ulinzi katika hali ya uchumi wako. uchmi wako unashikwa na akiba yako, ulinzi wa uchumi wako upo kwenye akiba. akiba yako itatoa tafsri ya namna gani utakabiliana na matatizo yatakayo husisha fedha. ukiwa huna akiba ujue huna ulinzi wa kifedha na kiuchumi, ila kuna kipindi unaeza ukatoa fedha yako yote ya akiba kwa ajili ya uwekezaji lakini pia katika kipindi hicho usisahau kuacha pesa kiasi ya kuweka kutumika kwa siku kadhaa katika matibabu na chakula.
katika hali ya kawaida ni lazima utenge asilmia 10 ya mshahara wako kama akiba ambayo haiwezi kuguswa kwa namna yoyote, lakini pia ni lazima uwe na account ya uwekzaji ambayo utapanga ni kiasi gani lakini isiwe wala isifanane na ailimia ya hapo juu, weka zaidi. sheria ya akiba nimsingo wa uchumi wako usiipuzee.
PANGILIA MAMBO YAKO MAPEMA, kuwa na ratiba yako ya matukio. watu ambao hawana karenda ya maisha yao kwa siku, wiki, mwezi na mwaka, hawa ndio huwa kwenye hatari kubwa na kushindwa kukabili matukio mabaya yanapo tokea matokeo, ukishindwa kujipanga ujiandae kufeli vibaya sana, kwasababu matukio mengi yanayo tutokea yanakuwa siyo mazuri hivyo sisi tuna wajibu wa kubadilisha hali hizo, na inawezekana pale endapo unakuwa na ratiba inayokuelekeza unapaswa kufanya nini na kwa wakati gani
KUWA NA UWEZO WA KUONA MAMBO KABLA HAYA TOKEA, Haya ni matokeo ya kuwa na maandalizi ukijua kujiandaa lakini kujiandaa huko kunatokana na kuwa na malengo ambayo yanakusaidia kujua mambo kabla hayajatokea. kwa mfano kulipa ada january siyoa ajali au siyo kitu cha ghafla hivyo unapaswa kujiandaa mapema lakini kwanini watu wengi wanaona kama cha ghafla kwasababu moja hawana tabia yakuweka akiba na hawana malengo yanayo zidi siku mbili, malengo ya leo na keshi haya uwezo wa kukufanya uwee kuona matukio ya mwaka ujao.
KUJUA NA KUTAMBUA ISHARA, Kila jambo katika maisha lina ishara zake, upofu tulionao unatufanya tusiweze kuona ishara hizo, upofu kwa maana ya kwamba uwezo wa akili kubambanua mambo umekuwa mdogo au haupo kabisa, kwasababu tumejifunza ku deal na matatizo yaliyopo mbekle yetu, na muda huo tu, ila hatujiongezi na kujaribu kuchunguza na kutimaza mikak 5 ijayo hali itakuwaje, kwa mfano kama wewe ni mfanaya kazi umeajiriwa hujawai kujiuliza nikifukuzwa kazi nitaishije? na hujatafuta njia mbadala mpaka sasa ya kusihi ujue wewe ni moja kati ya watu ninao wasema hapa.
jifunze kujiuliza maswali magumu leo, tambua maswali magumu na uyatafutie majibu, kukosa kwako majibu ndiko kunako pelekea ugumu mambo haya jitokeza kwa hali ya uhalisia na kukosa namna ya kuya kwepa zaidi tunalalamika na kukwama hapo, tatizo ulilinalo ukifanikiwa kulitatua ndo umetjirika kwa sababu mafanikio yako yamefichwa hapo. kazi ni kwako kutatua changamoto zako, kama huna hela tafuta sukuhisha la kukosa hela tena la kudumu, tafuta kila njia sahihi kuweza kumudu matukio yanayo kutokea kila siku.
itaendelea...................
Post a Comment