AMKA JITAMBUE

 

Robison Robison Author
Title: NAMNA YA KUTENGENEZA FEDHA ZAIDI-1
Author: Robison
Rating 5 of 5 Des:
        Katika maisha ni lazima ujue mbinu au namna ambayo unaweza ukatengeneza pesa zaidi, kukosa mbinu za kutengeneza fedha zaidi...

 

 

 Image result for money image

 

Katika maisha ni lazima ujue mbinu au namna ambayo unaweza ukatengeneza pesa zaidi, kukosa mbinu za kutengeneza fedha zaidi ni chanzo cha umasikini kwa watu wengi. hapa naamanisha umasikini wa kipato. umasikini wa kipato hutokana na kushindwa kutenegeneza fedha.

haijalishi wewe ni nani uko wapi unafanya nini, ila ni lazima ujue namna ya kutengeneza fedha zaidi katika maisha yako. jinsi ya kutengeza fedha hii ni sanaa ambayo kila mtu anaweza kujifunza na kuweza kuimudu tena kwa ufasaha.

kuna njia nyingi za namna ambavyo unaweza ukatengeza kipato. fedha inavya vyake ni lazima uvijue vyanzo vya pesa ukikosa kuvijua vyanzo au kuvitengeneza huwezi kupata fedha. lakini naomba ujue mpenzi msomaji swala la kutengeneza fedha siyo kazi rahisi na hakuna kazi rahisi hapa duniani kinachotakiwa ni kufuata sheria na kanuni zake.

zifuatazo ni njia utakzo weza kuzitumia katika kujua kwa namna gani unaweza kutengeneza kipato.

1.maarifaa. katika maisha yako hakikisha unakuwa na maarifa, kama unataka kuweka alama katika maisha haya baada ya wewe kuondoka ni lazima, utafute maarifa. swali maarifa yanapatikana kwa njia gani chanzo kikubwa cha maarifa ni kupitia njia ya kusoma. hakikisha unakuwa msomaji mzuri wa vitabu na majarida mbalimbali ambayo yanafanana au yana ujumbe ambao wewe unataka kuujua, lakini pia kwa kusikiliza na kuangalia vitu unavyotaka kujifunza.

kiwango chako cha mafanikio kinalingana  na maarifa uliyo nayo, nikimaanisha kiwaango cha vitu unavyo vijua vinalingana na uwezo wa mafanikio yako. ukijua vitu vichache hivyo ndivyo utakavyo kuwa, na ukiwa na maarifa ya kutosha utapata mafanikio yako. nataka ujifunze kutafuta maarifa kwa njia ya kusoma.

2. anza kufanyia kazi ndoto yako. njia ya kutengeneza fedha zaidi ni kutekeleza ndoto yako, fanyia kazi mawazo yako unajua au unayo kuwa na uhakika yata kuletea utajiri unao utaka, usiwe kikwazo cha mafanikio yako mwenyewe kwa kushindwa kuweka ndoto yako kwenye utekele zaji. kukwama kwa mafanikio tunayo yataka ni matokeo ya kushindwa kutekeleza mawazo au ndoto zetu, pale unaposhindwa kutimiza au kutekeza ndoto zako.

watu wengi tuna ndoto ambazo hatuziweki kwenye utekelezaji hivyo tunakuwaa na mawazo mengi ya kibishara lakini hatuyafanyii kazi kwasababu tunakuwa hatuna imani au hakika ya kwamba yatafanikiwa. kushindwa kujiamni kwamba haya mawazo yanaweza kufanikiwa huwezi kuwa na ujasiri wa kuyatekeleza.

jambo la msingi anza sasa kuyafanyia kazi mawazo yako utaona mabadiliko katika maisha yako. chochote unachofikiria kuhusu upataji wa fedha kifanye usisite site inawezekana, wote wenye mafanikio walianza kama wewe. anza leo azna sasa.

 3.jiamini na amini ya kwamba inawezekana. siri ya mafanikio yako imefichwa kwenye kujiamini kwako na kuamini kwamba inawezekana, amini kwamba unacho fanya ni sahihi na kitakufikisha kwenye mafanikio unayo yataka. imani yako inanguvu sana ya kuleta maono yako yatokee, usipokuwa mtu wa imani muda wote hujiamini, utapata kazi ngumu sana kufikia ndoto zako.

utekelezaji wa mawazo yako unategemea zaidi na kujiamini kwako katika kiwango chako cha kufanikiwa. huwezi kuwa mtu mwenye mafanikio kama utakuwa unashindwa kutekeleza kile unachokiamini. anza sasa kuekeleza mawazo yako hata kama yatapingwa, upinzani daima hua unatokea kwenye jambo jipya usikate tamaa fanyia kazi mawazo yako.

 

itaendeleaaa..... 

 Image result for money image

 

 

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top