kwanini watu hawapendi kujiamini kwenye yale wanayo yafanya. kuna sababu nyingi sana zinazopelekea watu kushindwa kuwakilisha vipaji vyao mbele za watu.
1. AIBU
kuna hili tatizo vijana wengi wanaona aibu kuonyesha vile walivyo navyo, ukishindwa kuonyesha kipaji chako au wazo lako ujue huna imani ya kutosha kwenye lile jambo unalo taka kulifanya. aibu ni ugonjwa wa watu wengi sana katika dunia hii ikimbie aibu uokoe hatima yako.
2. KUKOSA KUJIAMINI..
kwa lugha nyingine tunaweza kuita uoga, ukiwa ,uoga huwezi kuongea na watu ukiwa muoga huwezi kuwasilisha wazo lako au kipaji ulicho nacho. kinacho ficha mafanikio yetu ni uoga tulionao ndani yetu. tunaogopa kufanya hata vitu vilivyo ndani ya uwezo wetu, anza sasa kujiamini uone utakavyo tengeneza fursa. siyo kujiamini kwa mdomoni ila kwa vitendo.
3. MAANDALIZI MABOVU..
Ukosa maandalizi basi ujue umejiandaa kufeli, hakuna kitu kinacho fanikiwa bila maandalizi ya kutosha. hata kama una kipaji kikubwa kiasi gani lakini kama hujiandai vya kutosha lazima utakwama katika uwasilishaji, hakuna kinacho shindikana weka nguvu kwenye maandalizi.
Post a Comment