AMKA JITAMBUE

 

Robison Robison Author
Title: MATUMIZI YA PESA.
Author: Robison
Rating 5 of 5 Des:
  Ni rahisi sana kulalamikia matumizi yako kwamba ni baya, lakini nilicho gundua ni kwamba watu wengi, tuna fedha lakini tujil...

 Image result for finding money images












Ni rahisi sana kulalamikia matumizi yako kwamba ni baya, lakini nilicho gundua ni kwamba watu wengi, tuna fedha lakini tujilaumu sana namna tunavyo tumia.
kuna matumizi katika maisha ni ya kawaida ma mi ya lazima lakini kama kipato chako ni kidogo au kiwangoo cha hela unachotengeneza kwa siku au kwa mwezi hakilingani na mahitaji yako utajikuta mara zote unalalamikia matumizi yako lakini matumizi hayo ni ya lazima kwako na kwa kipindi hicho.

tatizo siyo matumizi tatizo ni wewe unapata pesa kidogo sana kiasi ambacho haitoshelezi matumizi yako, swala la msingi ni kutafuta fedha zaidi ila siyo kulalamikia matumizi yako au kupanda kwa gharama za maisha. tatizo la kupanda kwa gharama za maisha halitatuliwi kwa kulalamikia hiyo hali ila ni kujua namna ya kuzalisha fedha ya ziada ndiyo suluhisho la hali uliyonayo.

kulalamikia matumizi yako mara nyingi siyo utatuzi wa hali husika, mara nyingi watu hulalamikia matumizi yale ya msingi kwa mfano mtoto kaugua inatakiwa umpeleke hospital, zile gharama unazilalamikia swala hapa siyo gharama ila wewe unapesa kidogo na cha kufanya tafuta fedha zaidi ila siyo kulalamikia hali halisi ya matumizi ambayo huwezi kuikwepa kwa wakati huo.

chunga sanaa namna ambavyo unaitafsiri fedha katika maisha yako, usijeukailalamikia kwani kitu unacho kilalamikia unakuwa na maana ya kwamba hukitaki hivyo kinatoka katika maisha yako, usilalamikie pesa ila shukuru kwa kila matumizi unayoifanyia na iyone ni msaada katika maisha yako ila siyo tatizo. anza kushukuru kwa jinsi unavyo tumia pesa yako jione unatumia fedha yako kwa busara na kwa tija.

tafuta hela, weka mitega ya fedha, unacho takiwa kwa sasa ni kutengeneza fedha weka hela nyingi kwenye uwekezaji ili uweze kupata fedha zaidi. ukiwa na fedha ya kutosha utajikuta unaweza kumudu maatumizi yako kwa hkika utafurahia mahitaji yako kuliko kuya lalamikia.


TENEGENEZA FEDHA ZAIDI, UFURAHIE MATUMIZI YAKO..

 Image result for finding money images



 

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top