AMKA JITAMBUE

 

Robison Robison Author
Title: AKILI NI MTAJI
Author: Robison
Rating 5 of 5 Des:
  kiwango cha mafanikio yako kinapimwa na jinsi unavyo tumia akili yako, akili yako ndiyo kiwanda cha mawazo na kutengeneza fikra ambazo ...

 Image result for brain image

kiwango cha mafanikio yako kinapimwa na jinsi unavyo tumia akili yako, akili yako ndiyo kiwanda cha mawazo na kutengeneza fikra ambazo ndiyo nguzo ya kila kiwango cha mafanikio ambacho watu wengine wamekifikia au wewe mwenyewe unachotaka kukifikia.

hakika kwa kizazi kilicho jua mapema namna ya kutumia akili zao katika kufika kiwango cha mafanikio wanayo yataka, sasa hivi wako mbali na tunaona kama wanafanya vitu ambavyo haviwezekani katika macho ya kawaida. lakini ukweli ni kwamba wanatumia akili ileile ambayo mimi na wewe tunayo.

iliuweze kuona nguvu ya akili yako ili kutengeneza kiwango cha mafanikio unayo yataka ni lazima uamini kwamba akili yako yako inaweza kufanya na kukubadilishia maisha, hata kama itakuwa ngumu kuamini mara ya kwanza. ila endelea kujishawishi kwamba akili yako inauwezo wa kuzalisha mawazo ambayo yatakuwa bora na kukuletea mabadiliko unayo yataka.

huwezi kufikia mahali ambapo akili yako haijafika, kwa maana ya kwamba akili yako ndiyo jicho linaweza kuona vitu ambavyo havijatokea bado. ukiwa na uwezo wa ku IMAGINE kwa maana ya kwamba kuwa na uwezo wa kutengeneza taswira za maisha yako ya baadae ndiyo kiwango cha maisha unacho jipimia.

maisha yako unayatengeneza mwenyewe kupitia mawao yako, kwasabau wote tuna tenda kulingana na mawazo tuliyonayo. ukiwa na mawazo yenye kujenga na yenye kuleta suluhisho kwenye tatizo, ukishindwa kuleta suluhisho kupitia mawazo yako kwenye tatizo ulilonalo matokeo yake ni kujikuta umekwama eneo moja kwa muda mrefu.

anza sasa kuona au kuwa na njaa ya mfanikio, kuwa na kiu ya kutaka kuwa na mafanikio kupitia uwezo wa akili yako, watu wengi wanashindwa kuaminii kwamba akili zao zinaweza kuleta mafanikio ni sawa na mwanafunzi ambae haamini akili yake kwamba anaweza kufaulu bila ya kuiga kwa mwenzie, swala ni kwamba lazima uiamini akili yako kwamba inauwezo wa kutatua matatizo na kukufanikisha.

usipo kuwa na ujasili wa kujiaminisha ujue hutoweza kujiamini. kama hutoweza kujiamini huwezi kufanikisha lolote, ushindi upo kwenye kuamini yale unayo yafanya. na kujiamini huko kuna jengwa kupitia akili yako, lazima uiambie akili yako kwamba wewe unajimini na uiamini akili yako kwamba inaweza kukufanikisha.

TRUST YOUR BRAIN POWER, hakuna kitu kizuri kama kuamini kupitia akili yako hakuna atakae weza kukuyumbisha na kujiona yeye ni bora kuliko wewe amini kwenye njia zako unazo amini zitaweza kukufanikisha. kwasababu hakuna anaeweza kuamini jambo likiwa ndio linaanza. kubali kuanza peke ako ila amini kwamba utamaliza ukiwa na wafuasi wengi..

 Image result for brain image

 

 

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top