AMKA JITAMBUE

 

Robison Robison Author
Title: NGUZO YA ASUBUHI
Author: Robison
Rating 5 of 5 Des:
Kuna mambo ambayo unapaswa kuyafanya kila asubuhi mara tu amkapo, kubali kutumia akili yako kwanza kwa kujianda na siku nzima. kwanza kabisa...
Kuna mambo ambayo unapaswa kuyafanya kila asubuhi mara tu amkapo, kubali kutumia akili yako kwanza kwa kujianda na siku nzima. kwanza kabisa ni lazima uwe na malengo ambayo umekwisha yaandika, andika malengo yako na muda mzuri wa kuyasoma na kuya tafakari, muda mzuri wa kufikiria kuhusu mipango yako ni asubuhi, jifunze kutulia kwanza kabla ya kufanya kitu chochote jipange kwanza kwa kutafakari kwa umakini siku yako na mambo ambayo utakwenda kuyafanya.

acha kuishi kimazoea kwamba kila unapoamka we unakimbilia mswaki na kuoga then unakimbilia kazini, maisha ya aina hiyo wnaishi watu wengi tu na wewe ni shahidi aina hiyo ya maisha haija kufikisha mahali unapo pataka zaidi umejiongezea msongo wa mawazo unaotokana na kushindwa kufanikisha malengo yako na kuto ridhika na hali uliyo nayo sasa. unachotakiwa kufanya ni kubadilika pale uamkapo asubuhi.

asubuhi ndiyo huandaliwa siku, usianze siku bila kuipanga utafanya nini kwa siku hiyo husika, andaa ratiba ya matukio yote ya siku hiyo, lazima uwe unajua utafanya nini na kwa wakati gani kwa siku nzima hiyo hata kama ni kusoma ukurasa mmoja wa malengo yako, na hakikisha unaifuata ratiba hiyo.

jifunze kuamka mapema kwasababu ndiyo nguzo ya afya bora na mafanikio. hakuna tajiri duniani ambae akilala sa nne usiku anakuja kuamka kesho yake saa nne tena usipende sana usingizi, pumzika kwa muda unaofaa ili uweze kuamka muda unaofaa.

JIFUNZE KUAMKA MAPEMA.........................

 Image result for morning image
11 Mar 2016

About Author

Advertisement

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top