ukiweka malengo yako na ukiwa na kiu ya kutaka kufanikisha jambo fulani, ukakaza mwendo na kuweka nguvu zako katika jamb hilo ni lazima ndani ya miaka mitano utakuwa umelifanikisha. ukiona unaona kipindi cha miaka 5, ni kirefu sana ujue bado unaamini kwenye mafanikio ya haraka na huna uwezo wa kufikiri mbali. lakini ukiwa huamini katika mafanikio ya haraka na uamini katika mipango ya muda mrefu na ya muda mfupi basi huwezi kupinga nguvu ya miaka 5 katika utekelezaji wa ndoto yako.
uwe na mipango usiwe nayo katika kipindi cha hiyo miaka 5, lakini lazima miaka hiyo itafika tu hata ukiwa hai au umekufa lakini lazima miaka mitano itafika tu, hivyo huna haja ya kuishi bila ya kuwa na muelekeo wowote wa maana. ni vema na busara uka unatambua wapi unaenekea na weka nguvu nyingi sana kwenye wazo lako au kwenye kitu unachokitaka utafanikisha tu.
katika safari ya kutafuta mafanikio haina njia za mkato ukijiona unataka kufikia mafanikio yako kwa njia za mkato basi ujue hutafika mbali au hutayafurahia mafanikio yako kwa muda mrefu. kama wewe ni mfanya biashara baasi weka malengo ya miaka 5, ambayo utatakiwa kuyafikia ili kuifanya biashara yako iwe tofauti na ilivyo sasa, fikiria kuongeza idadi ya waanyakazi fikiria kuongeza mtaji wa biashra yako.
hata kama unakipaji ukikifanyi kazi mfululizo bila kukioma ndani ya mika mitano basi tayari na ni lazima jamii inayo kuzunguka itambue uwepo wako kwa kile unachokifanya, lakini siyo hivyo tu ukitaka kuishi au kutengeneza aina yoyote ya maisha unayoitaka inawezekana kufanikiwa ndani ya kipindi hicho.
changamoto ni kwamba watu wengi hawana muelekeo rasmi wa maisha ndiyo maana hividi vya mika mitano vimepita sanaa katika maisha yao na kushindwa kuleta tofauti yoyote ile, usiwe na mtazamo wa kuridhika na hali yako au usikubali kuwa tayari kuishi au kukutana na hali yoyote ile bila kukubali kutengeneza aina ya maisha unayoitaka. hakikisha unaweka mipango yako sawa ndani ya miaka mitano unaweza ukawa mtu wa tofauti kabisa.
kwamfano ukitaka kujenga ndani ya miaka 5 ijayo, anza kuweka akiba ya tshs 2000 kila siku ndani ya miaka 5 utakuwa na tshs 36m. kwa mfano ukianza kuweka mwaka huu mpaka kufikia 2020-2021 tayari utakuwa na milioni 36. ni pesa nyingi lakini imewezekana kwa kuweka tshs 2000 kila siku, jiulize ungeanza kuweka hiyo hela miaka 5, iliyo pita saivi ungekuwa wapi kimapato.
anza sasa inawezekana weka mikakati yako leo miaka 5 siyo mingi kama unavyo fikiria, jipange inawezekana. chukua hatua ya kuweka muelekeo wa maisha unayotaka kuyafikia tengeneza taswira unayotaka kuiona ndani ya miaka 5, ijayo fanya hivyo utafanikiwa sana katika maisha yako.
Sio kweli.. kapige mahesabu vizuri. 2000x30x12x5 haifiki hata 5M.
ReplyDelete2000 kwa mwezi ni 60000 tu (2000x30). Kwa mwaka ni 720000 (60000x12).. kwa miaka 5 ni 3600000 (720000x5).. unajengaje kwa milioni 3.5????