AMKA JITAMBUE

 

Robison Robison Author
Title: FURAHIA MATUNDA YA MAAMUZI YAKO.
Author: Robison
Rating 5 of 5 Des:
    Kinacho tugharimu ni maamuzi, pale unapofanya maamuzi na kuona matokeo chanya basi inakuwa ni mafaniko lakin pia kwa upande wa pili in...
 Image result for power image
 
Kinacho tugharimu ni maamuzi, pale unapofanya maamuzi na kuona matokeo chanya basi inakuwa ni mafaniko lakin pia kwa upande wa pili inakuwa ni changamoto kubwa unapo fanya maamuzi ambayo unakuja kujutia maamuzi yako. kila mtu angependa afanye maamuzi sahihi na yenye kumnufaisha na swali je, nitafanyaje maamuzi ambayo yatakuwa na manufaa na siyo hasara au yenye kuleta matokeo mabovu.

kwanza kabsa lazima tukubaliane kwamba kukosea katika maamuzi ni sehemu ya maisha, siyo kila siku utafanya maamuzi mazuri tu hapana ila tunachotakiwa kuona ni somo tunalolipata ili tusije kurudia makosa. kinachotakiwa ni kuto rudia makosa kwa kujifunza kutoka kwa pale tulipo kosea.

lakini siyo hivyo tu ni lazima tujifunze kufikiri kabla ya kutenda, ukifikiri kabla ya kufanya kitendo unapunguza uwezekano ,mkubwa wa kukosea au kufanya maamuzi mabaya ambayo badae utakuja kujilaumu. hakuna cha kupoteza katika kufikiri kabla ya kutenda fikiria kwa ufanisi hakikisha unakuwa na uhakika kiasi na kule unako elekea ujiridhishe siyo kufata simulizi tu na hadithi za wengine bila ya wewe mwenye kupata uhakika wa unachotaka kufanya.

usikate tamaa pale unapokosea kwenye maamuzi, kwasababu ni sehemu ya maisha kinacho takiwa ni kujipa moyo na kujifunza kupitia hayo ili uwe bora zaidi na kufikia mafanikio makubwa hapo baadae.
Image result for power image

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top