katika maisha yako kuna kipindi ambacho maamuzi yako yakua na matokeo ya papo kwa hapo, kila unacho fikiria kila unacho tenda kinakuwa na matoekeo kwa maana ya kwamba unapata kile unacho kitaka kwa wakati japo haijalishi ni kibaya au kizuri, lazima ujue nyakati unazopitia na kujipanga kufanya maamuzi sahihi.
umri wa kuanzia miaka 23 hapa tunaanza kuona matokeo ya tabia tulizo fundishwa tukiwa wadogo na wazazi wetu kwa maana kwamba makuzi ya le tuliyopewa tukiwa watoto ndiyo hasa tunayaanza kuyashuhudia yakifanya kazi kwa uhakika kwasababu hiki ni kipindi ambacho vijana wengi ndio huanza kujitegemea kwa maana ya kwamba kuwa na maisha ya bila uangalizi.
umri ambao unaanza kujiongoza wewe mwenyewe unajipangia ufanye nini uende wapi, kipato chako ukitumiaje bila kuulizwa na mtu yeyote. hapa ukishindwa kuwa na maamuzi sahihi lazima utapata matokeo mabovu katika uuzee wako kwasababu uwekezaji wako unafanywa katika kipindi cha ujana wako. katika umri ambao unatakiwa kufanya maamuzi sahihi ni kipindi ambacho unajiongoza.
kwasababu katika maisha kuna hatua 3, kwanza ya malezi ya wazazi lakini hatua ya pili ni hatua ya kujiongoza hasa pale unapo anza maisha ya kujitegemea na hatua ya tatu ni maisha yako ya kuwa na familia ambayo inakutegemea katika maamuzi na hatima yao ipo mikononi mwako chochote kibaya au kizuri utakacho kifanya kiitawathiri moja kwa moja.
ni lazima ujitambue uko wapi ili ufanye kila kitu kwa ufasaha kwa kulinganisha na nafasi uliyo nayo ili upate matokeo sahihi endapo utashindwa kujua nyakati zak utashindwa katika maamuzi ukishindwa katika maamuzi basi uwe na uhakika kuna mahali utakwama, tambua majukumu uliyo nayo, tambua fursa na nafasi ulizo nazo katika nyakati na uzitumie kikamilifu.
ukiwa katika hatua ya tatu ukashindwa kufanya maamuzi yenye tija kwa familia, matokeo yake ni kuiyumbisha familia nzima kwa maana ya kwamba maamuzi yako yatapelekea matokeo mabaya au mazuri, kwa kipindi hicho kila kitu unacho kifanya kinajionyesha hapo hapo, hata ukiamua kununua utaona hata unao waongoza nao wamenuna hata bila wao kujua huu ni wakati muhimu usibeze na hapo ndipo mafanikio yako yapo karibu sana kwasababu kila unachofanya kinatoa matokeo.
kuwa makini na nyakati, vijana wengi hupoteza dira kipindi ambacho waanza kujiongoza kwa maana ya kwamba mmaamuzi wanayofanya katika kipindi hiki yanakuwa haya tija sanaa wengi hujikuta wamesongwa na starehe na ansa za ujana ambazo huleta matumizi mabovu ya pesa kuliko uwekezaji wa kipato chao.
katika umri wa ujana una kazi kadhaa kwanza kuwekeza kipato na kufanya biashara, lakini pia kutengeneza familia.
tumia vema nyakati ulizo nazo ili uweze kuvuna matunda ya wakati huo.
Post a Comment