KUFIKIRI: JAMBO GUMU LAKINI MUHIMU
Niliwahi kumsikia Brian Tracy akifundisha juu ya “20 IDEA METHOD” ambapo unaandika njia 20 ambazounaweza kutumia kutatua tatizo ulilonalo. Mfano, tatizo la kifedha. Basi nikajaribu. Wakati huo nataka kutoa kitabu changu cha kwanza na mfukoni sikuwa na pesa mfukoni. Kwa kweli nilipoandika mpaka 5 nikaanza kusikia kichwa kinauma. Lakini kwa sababu alinitia moyo kwamba unapokaribia ya 20 ndiyo unapopata mawazo mazuri Zaidi. Nilifanya kwa bidii zote. Lakini mtindo huo ulinisaidia kupata laki tano kwa haraka.
Baadaye, nikaanza kuwapa watu wengine kila mtu akifika wazo la tano yuko hoi. Kwa kweli kuwaza sio jambo rahisi. Sio jepesi ila ni la muhimu sana. Na ukijizoea kuwaza sana kuna majibu utayapata ambayo wengi wanabaki na maswali.
Ukitaka kujaribu, Chukua karatasi andika kiasi cha pesa unachotaka kisha andika njia 20 zitakazokusaidia kuzipata.
TRY TO STRETCH YOUR BRAIN.
UTAGUNDUA UNA VYANZO VINGI SANA AU VIPAJI KIBAO..
Post a Comment