AMKA JITAMBUE

 

Robison Robison Author
Title: USIKATISHWE TAMAA NA HALI YAKO YA SASA..
Author: Robison
Rating 5 of 5 Des:
          watu wengi wanaogopeshwa na hali walizonazo sasa kiasi  ambacho wanashindwa kuamini kwamba kesho yao inaweza kuwa bora ...

 

 Image result for hope image

 

 

 

watu wengi wanaogopeshwa na hali walizonazo sasa kiasi  ambacho wanashindwa kuamini kwamba kesho yao inaweza kuwa bora kuliko leo.unaposhindwa kutambua kwamba unanafasi nyingine bora kabisa ya kufanya kesho yako ikawa bora zaidi ya leo usinge kata tamaa au kuona hakuna njia nyingine ya kufanya ufanikiwe.


binadamu katika maisha yetu daima tunakutana na changamoto mbali mbali ambazo kwa namna moja ama nyingine zinatukwamisha kuona maisha ya kesho kuwa bora kuliko ya leo.kitendo cha wewe kushindwa kuona kesho iliyo kuwa bora na yenye mabadiliko unafanya hiyo hali kuendelea kubaki kwenye maisha yako.


na kipimo kikubwa cha ukomavu wa mwanadamu ni kuendelea kuwa imara pale mambo yanapo haribika au mambo yanapokuwa mabaya. swala la msingi ni FOCUS yako inakuwa wapi hasa katika kipindi hicho, ukijiona unaangalia zaidi upande wa kushindwa na kuona ubaya tu, ujue unamtizamo hasi juu ya jambo hilo, lakini ukianza kuona uzuri wa jambo hilo basi utakuwa upo katika uwwezo wa kutafuta ufumbuzi na kushinda tatizo.

ni hali ya kawaida kila mtu kufurahi mambo yanapokwenda vizuri, lakini kila mtu anachukia jambo baya linapo tokea, lakini inabidi ujifunze kuto kufanya hisia na mawazo yako viendeshwe na matukio, hakikisha unakuwa na uwezo wa kumiliki tukio linapo jitokeza hakikisha unalimiliki kwa maana ya kulimudu hisia zako ziweze kumudu tukio.

kumbuka kwa kadri unavyoendelea kukaza fikra kwenye hali yako ya sasa unakosa mweleko wa kutengeneza kesho yako iliyo bora. matatizo yapo na kila mtu ynampata ila tofauti yetu ipo kwenye utatuzi kuna watu wanauwezo mdogo wa kutatua matatizo na kuna wenye uwezo mkubwa, lakin kila mtu anaweza kufikia kiwango cha juu katika kutatua matatizo kwa kuanza kuyakabili.

kumbuka hakuna hali ya kudumu kila jambo linakuja na lina pita tu, kwa kutambua hayo usikate tamaa endelea kusonga mbele haijalishi umekosea mara ngapi, haijalishi umekwama mara ngapi, haijalishi umepata hasara marangapi, haijalishi umekataliwa mara ngapi, unacho takiwa ni kukaza mwendo kuelekea mahali unakataka kufika. 


maisha ni uchaguzi, chagua kushinda na daima utakuwa mshindi...


Image result for hope image


About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top