“Kwanza
unatakiwa kujitambua wewe ni nani”, hii ni kanuni ya kwanza kabisa niliyo
inukuu kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Dar es Saalam, Mh Paul Makonda. Katika
kujijua na kujitengenezea fursa wewe mwenyewe ni lazima kwanza ujitambue wewe
ni nani. Bila kujua wito wako utahangaika miaka yote ukijaribu kufanya kila
jambo na kuona haliendi au haalisogei na kuto kuona motokeo ya jitahada zako
kwasababu moja tu unafanya kinyume na wito wako. Ni lazima ufike mahali
ujitambue wewe upo hapa duniani kufanya nini?
Ishara moja
kubwa ya kutambua mahali ulipo ni sahihi au siyo sahihi ni matokeo ya kile
unacho kifanya kuna watu wengi wamesoma na wanafanya kazi kupitia elimu zao
lakini huduma anayo itoa haifurahishi au haina ubora kabisa hata kama viwango
vyake vya elimu ni vikubwa, hili ni tatizo kubwa hapa inchini kwetu tunavijana
wengi walio soma lakini hatupati matokeo mazuri ya elimu zao kutokana na ukweli
kwamba walichosomea siyo wito wao wanafanya tu kwasababu ya pesa.
Stuka mapema
leo tambua uelekeo wako, tambua lengo lako la uwepo katika hii dunia hakika
hujachelewa wakati ni sasa chukua hatua ya kujigundua wewe mwenye na chukua
hatua za kutimiza ndoto zako, najua hata wewe mpenzi msomaji unafahamu umuhimu
wa mtu kugundua kipaji chake na namna gani kipaji kinavyo kuwa na uwezo wa
kubadilisha maisha ya mtu, sasa kwanini huchukui hatua na kutafuta nafasi ya
kutumia kipaji chako.
Tatizo ni
fikra, na mtazamo ulionao. Ukitaka kuelewa hapa namaanisha nini jiulize swali
hili ukisikia swala la kutambua kipaji akili yako inaona ni swala gumu au swala
rahisi. Kama bado hujagundua uwezo wako dhahiri lazima utakuwa unaona ni jambo
gumu sana na haliwezekani kirahisi labda mpaka atokee mtaalamu Fulani mwenye
elimu ya juu ndo aje akuonyeshe kipaji chako, jibu ni hapa huu mtizomo wako wa
kuona kuvumbua hazina ya kipaji chako ni swala gumu ndiyo unao kukwamisha
kufikia mafaniko yako. Ukweli ni kwamba kutambua wito wako ni rahisi kuliko
kitu chochote kile kwasababu kipaji hicho au wito huo upo ndani yetu hatuna
haja ya kuhofu katika hilo.
Changamoto
kubwa ni kwamba watu wengi hatuna muda wa kujitathimini, wa kujisoma na
kujitafuta sisi wenyewe ila tunakuwa bize zaidi na habari au na maisha ya watu
wengine kuliko ya kwetu matokeo yake tunajikuta hatuna muda wakitafakari sisi
ni akina nani au wito wetu ni upi, lakini pia hii hali inasabishwa zaidi na kuishi maisha ya mazoea kwasababu jamii
nyingi za kitanzania hazina utaratibu wa kukugundua vipaji au wito wa watoto wao,
hivyo basi tabia hiyo inaenda kizazi kimoja kwenda kizazi kingine na inaua
kabisa uwezo wa kujitambua.
Ndiyo maana
tunakwambia stuka mapema kwasababu katika jamii hizo hizo kuna vijana kama wewe
ambao wamekwisha kujitambua na leo hii tunaona makifanya vitu vikubwa taifa na
dunia kwa ujumla inatambua uwepo wao, kutokana na vile vitu wanavyo vifanya.
Kamwe usijione wewe upo katika hali ngumu sana kimaisha na huwezi kufanya
lolote au huna tena nafasi ya kufanikiwa, kwasababu njia bado zipo nyingi za
kukutoa hapo ulipo na wewe kukuza ndoto yako na kufanikiwa, wapo watu wengi
walio kuwa na hali kama yako, lakini leo hii wanaongea lugha ya tofauti kabisa
lakini ni baada ya kustuka mapema na kuchukua hatua, wakati wako ni sasa.
Kamwe
usikubali kuwa mtu wa kawaida kwamaisha yako, kwasababu hukuletwa hapa duniani
kuja kuzurura na kuwa mtu wa kawaida, hivyo basi kwanzia leo jiwekee viwango
vya kimaisha unavyo vitaka, jione ukiwa umefanikiwa na mwenye furaha kupitia
kile unacho kifanya. Kubali kukabili changamoto zote hakuna wa kukumisha wewe
kufikia ndoto yako, unachotakiwa tu ni kustuka mapema na kusonga mbele kutimiza
ndoto yako
Post a Comment