katika maisha ni lazima kifike kipindi ambacho utatakiwa kufanya maamuzi magumu ambayo kwa namana yoyote ile utawajibika katika hayo. utawajibika kimatokeo kama mazuri au mabaya, kwasababu ukitaka kufanikiwa inakubidi uchukue maamuzi hata kama hali uliyo nayo haikuruhusu ila inakupasa uchukue maamuzi na uanze kuyafanyia kazi, usitake kusubiri hali iwe shwari ndiyo uchukue hayo maamuzi.
ukiaona kitu unachokifanya sasa hakiwezi kukufanikisha au kukupeleka mahali unapo pataka basi huna budi kubadilisha muelekeo, tafuta njia nyingine ya kufikia ndoto zako usikae kwa kuogopa ugumu utakao kutana nao baadae. swala la msingi ni kuchukua hatua na kusonga mbele ili kutengeneza hatima ya maisha unayo itaka.
huwezi kujivunia mafanikio makubwa katika maisha yako bila ya kuwa na uthubutu wa jambo jipya kuwa na uthubutu huo anza sasa kutekeleza wazo lako la biashara, au jambo lingine lolote a,balo unadhani kwa kipindi hicho lina manufaa kwako. acha uwoga wa mazingira chukua hatua sasa anza kile kitu unacho kitaka kitokee au unacho fikiria kitakufanikisha.
usiwe mwenye kusita anza sasa fanya yale yaliyo ndani ya uwezo wako chukua hatua ya kiuhakika itakayo badilisha maisha yako, kama unawazo labiashara chukua uamuzi mgumu wakati wako ni sasa, usikae kutegemea siku au nyakati nyingine anza na kile ulicho nacha kifanyie kazi kwa ukamilifu.
ila jitahidi usifanye maamuzi kwa kurupuka, kuwa makini na maamuzi yako usifanya mambo kwa kurupuka hakikisha umefanya utafiti wa kutosha juu yajambo unalotaka kufanya utafiti wako ndio nguzo ya mafanikio ya mafanikio yako.
Post a Comment