kila mtu ana safari yake kuelekea mafanikio, lakini wachache sana wanatambua kama wapo sahihi na njia zao. wengi wanahofu na maisha yao kujiamini kwenye kile unacho kifanya imekua ndoto ngumu kufikika.
kama unataka kufanikiwa ni lazima utambue njia zako, ujue njia unayo pita ni sahihi kwako kuelekea mafanikio au hapana, kama utatambua kuwa unacho kifanya leo hakikupelekei kuwa tajiri wa kesho, kiache tafuta shughuli nyingine ya kufanya.
lazima moyo wako uwe na amani na akili yako pia ikubaliane na kile unacho kifanya ndipo utakapo ona mafanikio na kukubali kujifunza kwenye kila changamoto, na kuona ni sehemu ya kujifunza na kukua ila siyo kikwazo cha safari yako ya mafanikio.
elewa kile unacho kifanya sasa, kipende kile ulicho zaliwa nacho.
Post a Comment