watu wengi wanapenda kuwekeza fedha zao ili ziweze kuzalisha zaidi, hakuna ubaya katika hili kwa kuwekeza mahali iliuweze kupata zaidi na kuongeza kipato chako nadhani kila mtu anakuwa na lengo la namna hii ili kuweza kuboresha maisha yake.
lakini swala la msingi unakuwa makini kiasi gani ili usipoteze fedha zako kwenye miradi au biashara unazotaka kufanya, kwa kuepeka kutapeliwa au kuingia gharama nyingi zaidi zitakazo pelekea kupunguza faida na kupelekea hasara.
kama mtu yoyote anae hitaji kufanikiwa katika biashara hili ni somo la wazi kwa kila mmoja wetu kuhakikisha unajifunza na unakuwa na uwezo wa kutambua nini cha kufanya ili kukuza biashara yako.
moja ya mambo ya msingi kabisa ambayo unatakiwa kuyafanya ili kuweza kuwa makini katika uwekezaji ni yafuatayo
kwanza kabisa tafuta elimu ya kutosha juu ya jambo hilo, jaribu kusoma na kuwa tafuta watu walio bobea katika biashara ili wakupe uzoefu wao ambao utaweza kukusaidia katika kuanza jambo hilo.
jambo lingine ni kwamba kubali kuanza kidogo hata kama kwa wakati huo una mtaji mkubwa, usikubali ku risk fedha yako yote kwenye biashara mpya weka fedha kiasi zingine bakisha kama akiba kwamaana ya kwamba linaweza kutokea jambo loloye katika hiyo biashara litakaloweza kuhitaji fedha zaidi lakini pia kuwa na uwezo wa kuamka tena pale utakapo anguka.
uwezo wa ku negotiate, negotiations ni kitu muhimu sana katika biashara, kuwa na uwezo wa kubishana kwa hoja hasa pale unapokuwa unataka punguzo, daima watu waanza kukutajia bei iliyo juu kazi yako ni kuhakikisha unaishusha chini kwa gharama yoyote.jifunze ku bargain katika biashara ni lazima uweze hivi vitu viwili negotiations pamoja na bargain
kwenye uwekezaji hutakiwi kufika muafaka mara moja kama huna uhakika na hiyo deal kama huna uhakika au una wasiwasi nayo, jipange kuwa makini usiwe mwepesi kufikia maamuzi na uwe tayar kurudi kwenye majadiliano kama unahisi mwanzo umekosea, ila usifunge mjadala kama unahisi kabisa hiyo deal haikunufaishi, ni bora ukachelewa kuliko kuwahi lakini kwa hasara, ni bora usifanye kabisa hiyo deal kuliko kufanya then ukakwama au ukapata hasara.
lakini pia iliuweze kujua biashara flani ni lazima uingie uifanya ndo utajua mambo yote, wahenga wanasema ukitaka kujua utamu wa ngoma ingia ndani ucheze, na mimi nakwambia ukitaka kujua ujuzi wa baishara ingia uifanye.
Post a Comment