AMKA JITAMBUE

 

Robison Robison Author
Title: KUWA KAMA MMEA WA JANGWANI
Author: Robison
Rating 5 of 5 Des:
  Watu wote tunafahamu ya kuwa mimea inayomea jangwani hua mara nyingi inakuwa na tabia ya uvumilivu mkubwa kwenye ukame. lakini pamoja n...

 Image result for problem solving image

Watu wote tunafahamu ya kuwa mimea inayomea jangwani hua mara nyingi inakuwa na tabia ya uvumilivu mkubwa kwenye ukame. lakini pamoja na ukame huo hiyo minea huweza kuhimili kwa kiasi kidogo sana cha matone ya mvua kinacho patikana kwa mwaka.

nimetoa mfano huo nikiwa na lengo ya kufananisha mmea wa jangwani kama mtu ambae anakubwa na matatizo na changamoto za hapa na pale ambazo kimsingi ndiyo sehemu ya maisha yetu. hakuna mwanadamu  ambae toka anazaliwa aishi bila kukumbana na changamoto.

sasa ni watu wachache sana wenye uwezo wa kuhimili misuko misuko ya kimaisha, na kukubali matokeo ya kwamba yale matukio yanawazidi uwezo na kubaki wakilalamika na kushangaa kwanini mamba yanakuwa hivyo yalivyo bila ya kuchukua hatua yoyote.

mmea wa jangwani unatabia ya kuwa na mizizi mirefu pamoja na kuwa na uwezo wa kupukutisha majani, ili kuweza kuhimili ukame. kumbe katika kipindi cha matatizo na changamoto zetu ni lazima tuwe na mbinu sahihi za namna ya kuweza kupambana na kufanikisha malengo yetu.

kamwe huwezi kufanikiwa bila kukumbana na vikwazo mbalimbali vya kimaisha ni wajibu wako kujituma na kufahamu nini cha kufanya ili kutatua matatizo yanayo endelea. na kwa kufanya hivyo unatengeneza mazingira ya kufanikiwa.

jaribu kuangalia uwez wako ili kutatua matatizo yanayokuzunguka kwani ndiyo ngazi yako ya mafanikio, kiwango cha mfanikio yako kinapimwa na uwezo wako wa kutatua matatizo. be a problem solver
Image result for problem solving image

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top