Maisha yana kanuni, na maisha yana sheria zake, ni lazima ujue kwamba kitu unachofanya kitakufikisha katika mafanikio au la, usifanye kitu kwa kubahatisha inabidi uwe unajua nini unafanya na unataka kwenda wapi na tabia yako.
zifuatazo ni hatua au mambo matatu muhimu kuyafanya katika maisha yako
1. MBINU ZA KUTAFUTA PESA
au kuwa na elimu ya fedha katika maisha yako, ni lazima ujifunze kwa uhakika kabisa kwa kusoma, kuhudhuria seminar zinazo husiana na maswala ya fedha. ukisha jua namna ya kupata fedha katika maisha yako tayari unakuwa na uhakika wa kuishi maisha yenye nafuu.
lakini kujua kupata pesa kuna ambatana kwa ukaribu na mbinu za kufanya biashara, ili uweze kufanikiwa kifedha ni lazima uwe mfanya biashara, ni lazima uwe na mbinu sahihi za kibiashara ili uweze kufanikiwa kifedha, hakuna ambaye anaweza kusema kafanikiwa.
2. KUJISOMEA
ukitaka kusogea mbali na maisha yako na kuweka zaidi ya mgodi unao tembea ukiwa na uhakika kwamba ndoto zako zinaweza zikatimia, huwezi kufanikiwa kwa akili yako na aina ile ile ya kufikiri. lazima uweze kubadilika namna ya kufikiri ili uweze kuona possibilities za kufanikiwa katika maisha yako.
3. KUANDIKA MALENGO YAKO
huwezi kufika mahala usipo pajua, lakini pia huwezi kufika mahali usipo pataka, lazima ujue kwamba malengo yako ni muhimu sana, hasa kwa kuweka hali sawa ya muelekeo wako kimaendeleo, kwa kujua nini unatakiwa kufanya na kwa wakati gani.
kila siku weka malengo yako, kwasababu mafanikio ni mjumuisho wa mambo madogo madogo ya kila siku. yale unayo yafanya kila siku ndiyo yanayo kupelekea kwenye mafanikio.
Asante sana kwa Ujumbe mzuri
ReplyDeleteahsante sana edgar kama umepata cha kujifunza. nikutakie mafanikio mema
Delete