AMKA JITAMBUE

 

Robison Robison Author
Title: TABIA TANO ZA MATAJIRI
Author: Robison
Rating 5 of 5 Des:
  leo nimeona ni vema nikakuletea tabia za matajiri, ambazo hata wewe unaweza ukajifunza au kuaanza kuzifanyia kazi kwasababu ziko nda...
 Image result for five image





leo nimeona ni vema nikakuletea tabia za matajiri, ambazo hata wewe unaweza ukajifunza au kuaanza kuzifanyia kazi kwasababu ziko ndani yako  kwasababu umeumbwa kuwa tajiri na siyo masikini na ndio maana kila mmoja wetu anauchukia umasikini na kutaka kuwa tajiri au kuishi aina ya maisha yenye uhuru ambao yeye anautaka.

zifuatazo ni njia kuu ambazo matajiri wanazitumia kila siku na kuwa fanya wawe hapo walipo leo.

 MTAZAMO CHANYA. hii ndiyo silaha kubwa ya watu walio fanikiwa kifedha na katika nyanja nyingine yoyote, wanakuwa na mtizamo chanya kwenye kila kitu wanachokifanya  hofu ya kushindwa ni ndogo kuliko nguvu waliyo nayo katika kufanikiwa. daima mtu mwenye hofu nafasi yake ya kufanikiwa ni ndogo na daima mahali penye ujasiri mafanikio ni lazima.

UWEZO WA KUTENGENEZA VITEGA UCHUMI, watu walio fanikiwa wanakuwa na tabia ya kutengenza vitega uchumi, vitega uchumi ni vitu ambavyo vinakuwa na uwezo wa kuzalisha pesa kwa tasfiri nyingine mtu mwenye mafanikio kifedha huwa daima hana chanzo kimoja cha kimapato, usiwe na chanzo kimoja cha mapato.

kosa wanalolifanya watu masikini ni kwamba wanakuwa na chanzo kimoja au hawana kabisa chanzo cha mapato. hilo ndilo kosa kubwa  na huo ndiyo mwanzo wa umasikini.

KUTENGENEZA MARAFIKI WENYE TIJA, matajiri wanatabia ya kutengeneza marafiki wenye tija marafiki ambao wanauweza kubadilisha hali za maisha yao kwa ushauri na kupeana mawazo mapya ya kibiashara, lakini ni tofauti kwa mtu masikini yeye anajenga urafiki na watu ambao wanawapa mabo ya kufuraisha tu kama umbea na vichekesho lakini mambo ya kujenga na kuonya hawana muda nayo. masikini wanakuwa na marafiki wengi ambao ni mzigo na wana siyo msaada kwenye maish ayao.

UWEZO WA KUJIFUNZA NA KUTAFUTA TAARIFA SAHIHI, watu walio fanikiwa daima wanakuwa na tabia ya kutafuta taarifa tena siyo taarifa tu ni taarifa sahihi ambazo wanajua zinauwezo wa kubadilisha maisha yao, kwa kusoma, kusikiliza na kutizama wanakuwa makini kwenye vyanzo vyao vya taarifa na wanawekeza mahali ambapo wanaweza kupata taarifa sahihi.

UWEZO WA KUWEKA MALENGO, watu wengi wanaishi bila malengo ni wepesi kuyasema kwamba nna malenho lakini kiukweli hakuna walicho kiandika, huwezi kusema unamalengo bado yakawa kichwani tu malengo ni lazima uyaandike. hiyo ndiyo tofauti ya masikini na tajiri.


About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top