Huwezi kufa kwa kuzama ndani ya maji ila unakufa kwa kubaki ndani ya maji,
watu wengi tuna airisha sana kuishi, tunasema kila kitu tutafanya kesho na kwa bahati mbaya kesho huwa haifiki. lakini baadae siku zinaenda, zinakuwa wiki, wiki unakuwa mwezi, mwezi unakuwa mwaka, mwaka inakuwaa miaka kuja kushangaa tumeshakuwa watu wazima.
kumbuka hili hakuna siku za ziada, na siku sahihi kufanya maamuzi ni leo,acha woga fanya lile ambalo kwako ni la msingi anza kufanya sasa na leo.
njia ni kama zifuatazo.
1. andika mambo yako 20, unahisi ni muhimu katima maisha yako, kwa kufanikisha au kuishi kwa kiwango unacho kiona utajihisi umefanikiwa. iwe katika kazi, biashara, ama kipaji chako.
2. tumia muda mwingi kufikiria, watu walio fanikiwa katika maisha yao huwa na muda wa kufikiria nini wanatakiwa kufanya sasa ili kuendeleza maisha yao wenyewe na kufikia mahali wanapo pataka katika maisha yao.
3. kuwa na usawa kati ya maisha yako binafsi na familia yako, usijikite sana kwenye kazi na biashara zako na kusahau familia yako, weka usawa huo katika maisha, usije ukasahau familia yako, hiyo ni zawadi toka kwa MUNGU itunze na kuieshimu.
4. kuwa mtu wa kujifunza mambo mapya kila siku, chukua mazoea ya kujaribu mambo ambayo hapo mwanzo ulio hayawezekani anza kujifunza, utaona mabadiliko katika maisha yako.
5. kuwa na moyo wa upendo, waonyeshe watu wengine upendo, hii siyo ishara ya uwoga ama uzembe ila ni ishara ya kujitambua na kuwa na akili ya kutambua mdhaifu na uwezo wa watu wengine.
6. kuwa tofauti, isiishi maisha ya kuiga watu wengine ishi kulingana na matakwa yako na misimamo yako. usiwe mwepesi wa kufuata mkumbo.
kufanikiwa ni lazima, hutakiwi kukata tamaa katika maisha yako.
Post a Comment