siri ya mafanikio ya mwadamu imejificha kwenye jambo moja kuu, nalo ni kufanya kile unachokipenda, kwasababu watu wengi wanashindwa kufanikiwa kwa kukata tamaa. ndoto za watu wengi zimeshindwa kuishi kutokana na ukweli kwamba wahusika walikuwa wakikata tamaa.
sasa ukiwa unafanya jambo ambalo unalipenda unatoa uwezekano wa wewe kukata tamaa na kama huto kata tamaa basi mafanikio ni yako.
lakini pia kikwazo kingine cha watu kufanikiwa ni kushikwa na matukia yaiyo pita, tunaishi na machungu ya hasara zilizo pita, tunaishi kwenye mazingira magumu kwasababu sisi wenye tumeruhusu kwa kuona hatuwezi kubadilisha hali hizo.
matukio yaliyo pita haya tafsiri hatima yako, ukizembea kuchukua hatua na kuacha hofu ya maisha yako yaliyo pita ikusumbue na kuona huwezi kufanikiwa, basi kutakuwa hakuna namna nyingine ya kutoka hapo ulipo na wewe kuwa mtu wa tofauti.
ili uweze kufanikiwa katika maisha yako ni lazima uwe na ramani ya unako taka kwenda tena iyo ramani iandike kabisa, na itengeneze kwa ubora unautaka, kwa kuiandika unataka maisha yako yaweje, baada ya hapo anza kuweka misingi kwa kufanyia kazi mipango yako.
usiwe na mipango ya mdomo inakupasa uandike, elezea nini unataka katika maisha yako, halafu chukua hatua ya kutekeleza malengo yako.
Post a Comment