kila siku katika maisha tunakutana na nyakati ngumu, nanyakati hizi ndizo zinazolete matatizo katika maisha, kwani pale tunaposhindwa kuzitatua zinageuka kuwa matatizo.
kwanza kabisa nyakati ngumu huwezi kuzikwepa ila tutafuta namna sahihi ya kuzimudu na kufanya zisitumize au kutuharibia maisha yetu na matarijio yetu kabisa.
nini tunatakiwa kufanya,
1. tunapo ingia kwenye changamoto kwanza hatutakiwi ku panic au kuhamaki, kwasababu ukifanya hivyo unajima muda wa kufikiria, lakini pia huwezi kupata majibu mazuri ukiwa umesha hamaki, inaweza ikatokea ukahamaki lakini kumbuka kutafuta utulivu. weka akili kwamba inakubidi utulie ili uweze kutatua tatizo
2. jifunze kuishi kwa tahadhari, usiishi bila kuwa na taharadhi, ishi ukijua lolote linaweza kutokea, ishi kwa kujiamini lakini pia weka tahadhari, jua lolote linaweza kutokea na ukisha jiandaa chochote kikitokea unaweza ukamudu kwa kuvumilia kwasababu akili yako ulisha iandaa.
3. usiishi kwa kuwategemea watu,usije ukaweka imani yako kwa watu, marafiki, au ndugu. wote hawa wanaweza kukuangusha kwa namna moja ama nyingine. mtu wa kwanza kuweka imani kwake ni wewe mwenyewe, jiamini kwamba wewe unaweza kubadilisha matokeo, lakini pia muamini MUNGU kwamba yeye anaweza kubadilisha hatima yako.
4. tumia vizuri nyakat nzuri zako, kila mwanadamu huwa anapata nafasi ya kuwa na wakati mzuri, kupata fursa, nafasi ya ku shine nk. kwa uzembe wetu huwa tunajisahau tukidhani mambo yataendelea kuwa mazuri hivyo hivyo, lakini pia kuna watu hawatambui kwamba wakati mzuri ni upi, badala yake wanakuja kuutambua muda ukiwa umepita. point ya msingi hapa ni kuhakikisha unatambua nyakati yako nzuri na kuitumia vema.
5. jifunze kuwekeza kwa watu wengine, watu wengi ni wachoyo na wabinafsi, hicho kitu kinapelekea kwamba hata wao wanapopata shida kushindwa kupata msaada kwasababu wao wenyewe hawana utaratibu wa kusaidia wengine.
zinagatia haya lakini zaidi kumbuka kutoa zaka katika pato lako ili kuhakikisha ulinzi wa KIMUNGU kwenye maisha yako na kwenye kipato chako.
Post a Comment