AMKA JITAMBUE

 

Robison Robison Author
Title: AINA TANO ZA MITAJI
Author: Robison
Rating 5 of 5 Des:
AINA TANO ZA MITAJI Na Robison Sisyan Watu wengi tunashindwa kufanya vitu katika maisha yetu kutokana na ukweli kwamba tunalia hatu...


AINA TANO ZA MITAJI
Na Robison Sisyan
Watu wengi tunashindwa kufanya vitu katika maisha yetu kutokana na ukweli kwamba tunalia hatuna mitaji, siyo hivyo tu watu wengi wamekwisha sema ukisema unatafuta mtaji ujue wewe ndiyo mtaji wa kwanza. Sasa wewe unwezaje kuwa mtaji au ni kitu gani kinakufanya wewe uwe mtaji.

Leo tutajua sababu ambayo inakufanya wewe uitwe ni mtaji wa kwanza na unaposema unatafuta mtaji ujue unajitafuta wewe mwenyewe na kujua tu unatumiaje ulivyo navyo ili kufanikiwa katika maisha yako.

Kiu yetu ni kuona mafanikio katika maisha yetu, lakini kwenye hii safari ya kufikia malengo yote, kuna vitu tunajikuta hatua, na hivi vitu huwa ni muhimu sana kufikia malengo yetu, kimoja wapo ni kujitambua. Ukijitambua wewe ni nani uko wapi, na unatakiwa kufanya nini.

Zifuatazzo ni aina za mitaji ambazo kila mwanadamu anazo, kinachotakiwa ni kuzitambua na kuanza kuzianyia kazi ili zikuletee matokeo mazuri.

Uhai, kama unasoma makala hii, ujue unanafasi ya kufanikiwa katika maisha yako, mtaji wa kwanza ni uhai, huwezi kufanya jambo lolote ukiwa ni maiti, ukiwa hai ndiyo uaweza ukafanya na ukatenda na vitu vikatokea, hivyo huna budi kujikita katika kuthamini uhai wako kwa kuutumia ipasavyo ili uweze kufanikiwa.

Afya, mtu mwenye afya njema anauwezo wa kushiriki shughuli yoyote ya uzalishaji na kwa ukamilifu, ukiwa hauko timamu kiafya huwezi kutekeleza majukumu yako hata ukiwa na nia ya kufanya hivyo, hivyo basi afya tulizo nazo ni mtaji tosha kwasababu tunaweza tukaamua cha kufanya kwa wakati wowote na kikawa.

Akili, mtaji mwingine ni akili, hapa tunazungumzia utashi, uwezo wa kutambua na kuelewa, wewe ni nani uko wapi, na unatakiwa ufanye nini, kwenye akili ndiko kwenye hazina ya majawabu ya maswali yetu. Ili akili ipate nafasi ya kufanya kazi vizuri  ni kazima iwe na maarifa, kazi unayotakiwa kuwa nayo katika maisha yako ni kujaza akili yako maarifa ya kutosha.

Uwezo wa kufikiri, kila mtu kajaliwa uwezo wa kufikiria, kwenye kufikiria kwa ufasaha na kwa ufanisi kunahusisha zaidi akili yenye maarifa. Mtu anae jua kufikiri vizuri ni lazima ajue kupanga na kweka mikakati dhidi ya maisha yake mwenyewe, huwezi kufanikiwa kama hutengi muda wa kufikiri na kuweka malengo katika maisha yako, swala ni wewe kuamua kuanza kufikiria ili upate jibu la matatizo yako.

Uwezo wa kuamua, ulichokifikiria katika akili yako ilikitokee ni lazima ufanye maamuzi ya kuchukua hatua ya kuyatekeleza, usiishe kuwaza na kufikiria pekee chukua hatua na kuyatekeleza maamuzi yako. Hapa kwenye kuamua ndiyo kwenye utendaji anza na kile ulichonacho kukamilisha mawazo yako ili kufikia ndoto yako.

Huu ndiyo ukweli na hazina zilizo jificha katika maisha yetu, hii ni mitaji na ndiyo nguzo kuu za mafanikio, hakuna mafanikio yanayotoka nje ya haya mambo matano na ukisha jua jinsi ya kuyatumia haya ndipo utakapo jigeuza wewe mwenyewe kuwa mtaji, lakini pia ndipo utakapo jigeuza wewe mwenyewe kuwa mtaji na kuweza kuzalisha mali na utajiri katika maisha yako.
Amkajitambue.blogpot.com
+255 653 206 053

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top