unajua mafanikio ni mtazamo, kushindwa au kufauli ni mtazamo, ila siyo facts au siyo ukweli huo ila sisi ndiyo tumeweka viwango vya mafanikio na kitu ambacho siyo mafanikio.
na kila mtu amefanikiwa lakini pia kulingana na viwango na vigezo alivyojiwekea yeye mwenyewe ambavyo vinatokana na vitu alivyo jifunza na alivyo jifunza kuhusu mafanikio.
sababu kubwa inayokufanya ujione hujafanikiwa ni kwamba unajilinganisha sana, lakini pia wewe hujui upo kwenye hali gani, au unataka kufanikisha nini kwenye maisha yako, lakini pia kuishi kwa kujilinganisha sana, japo haikatazwi kujifunza kutoka kwa wengine.
kinachotakiwa ni kubadilisha mtazamo, anza kujiona kama mtu ambae unauwezo wa kutengeneza hatima chanya ya maisha yako, mtu ambae unauwezo wa kuishi na kutengeneza ndoto za maisha yako.
mtaji wa kwanza wa mwanadamu katika kuelekea mafanikio yake ni akili, akili ambayo inaendeshwa kwa maarifa na maarifa yanayopatikana kwa njia ya kusoma, kusikiliza na kutazama.
wekeza kwenye akili yako kwa matokeo bora ya maisha yako,
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.