huwezi kufanikiwa bila kuwa na malengo, ili ujione umeefanikiwa ni lazima uwe umejiwekea kiwango flani cha kufikia mafanikio na wewe kuvuka kiwango hicho. malengo halisi na ynayo tekelezeka ni lazima yawe na sifa kadhaa za muhimu ikiwemo
1.malengo ni lazima yaandikwe
2.lazima yawe na muda wa ukamilifu au ukomo
3.malengo ni lazima yaandikwe katika wakati uliopo
hizo ni baadhi ya sifa za malengo ambayo yanaweza kutekelezeka na wewe kukuletea mafanikio, watu wengi wana malengo lakini malengo hayo yapo kichwani tu haja andikwa, sasa unapokuwa na lengo ambalo hujaliandika ni rahisi kuyumbishwa na utashindwa kujipima kama kweli umelifanikisha na kwa kiasi gani huwezi kufanya tathimini, lakini katika jamii ni vijana asilimia 3 tu wenye malengo yaliyo andikwa.
jifunze kupanga vitu vyako mapema, kwasababu dk 1 katika kujiandaa inaokoa dk 10 katika utekelezaji, lakini siyo hivyo tu ukipanga siku yako mapema unakuwa unajipa wewe mwenyewe uelekeo wa kwamba unatakiwa kufanya nini na kwa wakati gani. huwezi ku FOCUS ikiwa huna muelekeo kamili wa kufika unako taka kwenda.
mfano kama unataka kufikiwa billionaer ndani ya mika 10 au 20 ijayo, igawanye hiyo miaka katika vipindi vifupi vifupi ili uone kazi ambayo utatakiwa kuifanya kila siku ili uweze kufikia lengo lako kuu, malengo yetu ni lazima yatimie kwa kuyafikia kila mara na kujenga taswira ya jinsi yalivyo kwa kufanya hivyo unaihusisha akili yako ili iweze kukutengenezea mazingira mazuri ya wewe kufikia malengo yako.
Post a Comment