AMKA JITAMBUE

 

Robison Robison Author
Title: NEVER GIVE UP
Author: Robison
Rating 5 of 5 Des:
  Watu wengi katika maisha wanakatishwa tamaa na matukio au mambo yanayo tokea, katika safari yao ya maisha. ninacho taka kukumbusha tu n...

 Image result for motivation image

Watu wengi katika maisha wanakatishwa tamaa na matukio au mambo yanayo tokea, katika safari yao ya maisha. ninacho taka kukumbusha tu nikwamba kamwe hutakiwi kukata tamaa, ukikubali kushindwa na majaribu au matatizo yanayo kukabili, hivyo utaendelea kuishi kwenye aina hiyo hiyo ya maisha kwasabau utakuwa umeamini na kukubali kwamba umeshindwa.

daima kuwa mpambanaji mpaka mwisho  hakuna cha kukukwamisha zaidi yako, haijalishi unapitia vitu vingapi ila endelea kuamini kwamba wewe ni bora zaidi ya changamoto zinazo kuzunguka na unaweza wa kuzishinda na kuwa bora zaidi.

na ukweli wa maisha upo hivi kwa kadri unavyo shinda changamoto ndivyo unavyo zidi kuwa bora na kukua zaidi, na uhalisia uko hivi yule mtu alie fanikiwa zaidi ndiye huwa anavuka chamgamoto zake kwa mafanikio, na wewe ukitaka kufanikiwa vuka changamoto zako kwa mafanikio.

wengi wanaharibikwa na matatizo au shida zinazo wakuta, wanaharibikiwa na hayo mambo yote na kujikuta wanapoteza muelekeo kabisa katika maisha yao, usipotezwe muelekeo na matatizo, lengo la hayo ni kupima uwezo wako na ni lazima uonyeshe ukomavu mbele ya tatizo.

watu wengi huwa wanyonge mbele ya shida zao, wengi wanakubali uhalisia wa matatizo hayo na matokeo yake hizo hali haziwezi kutoka kwasababu zinaogopwa na wahusika kwa kuonekana ni kubwa kuliko wao. usilinyekee tatizo komaa mpaka uliondoe.

anza kuwa mbabe mbele ya matatizo yako, yaonyeshe unaweza, yaonyeshe we ni jeuri na unaweza kuyashinda.


.Image result for motivation image

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top