kila siku hakikisha unakuwa kama mtu mpya, weka mambo matatu ya kukutia moyo, ya kuipa akili yako muelekeo, unajua unafahamu ya kuwa binadamu tuna uwezo wa kuamua na kufanya kwa mafanikio jambo lolote ambalo unataka kulifanikisha.
watu wengi tunaamka na hali mbaya ya jana tunasahau kwamba leo ni siku mpya ambayo hajawai kuwepo tangu kuumbwa kwa huu ulimwengu, hivyo hatuna budi kuwa wapya pia kusahau hali mbaya tulizo kutana nazo jana kwa kujipa moyo na kujiambia vitu unavyo vitaka maishani.
sasa jenga kile unacho kitaka kwenye akili yako, kiseme, kiwaze, kifikirie mara kwa mara, jenga mtazamo wa ushindi katika maisha yako.
jiaone unaweza kufanikiwa yale unayo yataka katika maisha yako, jione ni mshindi na sio msindikizaji, usikubali kila siku kukubali kuwa msikilizaji taka siku moja uwe msimuliaji, wa mafaniko, na kutoa story za miji iliyoendelea duniani, uwe mtia moyo siyo kila siku ufundishwe wewe tu na utiwe moyo wewe tu.
Post a Comment