swali kubwa la mtu yoyote ile ni namna gani ataweza kutengeneza faida kwenye biashara, namna gani ataweza kutengeneza mazingira ya kufikia hilo lengo lake, hapa mpaka imani potofu zimeingia kwa baadhi ya watu kuamini kwamba nguvu za giza ikiwa namaana kwenda kwa ganga ni sehemu ya kufikia mafanikio ya kibiashara.
sasa ni lazima ujue nini kinatakiwa kufanyika ili kufikia uwezo wa kutengeneza aina hiyo ya faida unayoitaka, ili kuweza kukuza biashara yako.
kwanza fikiria jambo linalo kupa faida, unafanyaje kutengeneza faida yako ya sasa, angalia chanzo cha faida yake kiko wapi, hapa mimi siwezi kuandika vyanzo vya faida katika biashara, ni vingi sana kutegemea na biashara unayo ifanya. biashara unayo ifanya ichunguze ikupe aina jibu la chanzo cha faida theni kimaarishe chanzo hicho.
hatua ya pili fanya biashara ambayo utalipa kodi ndogo zaidi, kama ndiyo unaanza biashara usianze biashara ambayo kodi yake ni kubwa sanaa itakupunguzia kiasi cha faida yako, fanya biashara ambayo kiwango chake kwa kusumbuliwa na kodi ni kidogo, mfano biashara ya kilimo, na kilimo chenye.
lakini pia faida inapatikana kwa kununua bidhaa unazo uza kwa bei nafuu, ukinunua bidhaa kwa bei ya juu itashindwa kuuza, tafuta namna ya kutafuta bidhaa zako kwa bei nafuu kabisaili uweze kuuza vizuri na kutengeneza faida kubwa.
ongeza ubunifu katika usambazaji, kusambaa kwa bidhaa au huduma yako kwa wingi kuna faida au mchango wa kukuongezea wateja hivyo tunategemea kukuongezeka kwa uuzaji wa bidhaa hivyo kuendelea kutengeneza faida zaidi.
tatua tatiza kwa jamii, ukitatua tatizo ambalo lilikuwa kero na ukaonyesha msaada kwa watu wengine basi utakuwa na nafasi ya kufanikiwa zaidi kibiashara, usiuze kitu bila kujua uhitaji, peleka mahali penye ulhitaji wa uhuduma au bidhaa yako.
Post a Comment